Feb 15, 2025
09:00 AM
St. Gaspar, Dodoma

Secretarieti ya Mzumbe Secondary School Students Alumni Association (MSSSA) inapenda kuwatangazia kwamba Mkutano Mkuu (AGM) wa mwaka 2024 utafanyika Jumamosi tarehe 15 Februari 2025, katika ukumbi wa St. Gaspar, jijini Dodoma, kuanzia saa 3 asubuhi.
Ajenda za mkutano wetu zitakuwa kama ifuatavyo;
1. Kupitia kumbukumbu za kikao kilichopita na yatokanayo na kikao hicho
2. Taarifa ya chama kwa mwaka 2024
3. Kupitisha taarifa za fedha zilizokaguliwa kwa mwaka 2023 & 2024
4. Uchaguzi wa Viongozi
Sambamba na mkutano huu, kutakuwepo shughuli za michezo na starehe kwa lengo la kufahamiana na kujadiliana mambo mbalimbali.
Tunawaomba Wazumbe wote tufike kwa pamoja na tushiriki ili tuweze kujadili mambo yetu na kuujenga kwa pamoja Umoja wetu.
Mkutano huu ni kwa ajili ya wanachama wa MSSSA waliosajiliwa.
Gharama za siku ya mkutano, ambazo ni pamoja na ukumbi, chakula cha mchana na cha jioni na viburudisho zimegharamiwa na Alumni. Wajumbe wanaombwa kujilipia gharama za usafiri na malazi. Kuna bei ya punguzo kwa watakaopenda kulala St. Gaspar.
Zoezi la kupata uthibitisho wa ushiriki linashughulikiwa na Kamati ya Mambo ya Jamii. Tunatanguliza shukrani kwa ushirikiano wenu.
TUPO PAMOJA, TUPO PAZURI.
Edward Zakaria Talawa
Mwenyekiti
Register the biggest Network of Talented Alumni Students in Tanzania. Connect for Professional , Social and Business Connection. Determination is our Motto.